×
×

Kuwa na Pindi Zinazofurahisha

Swahili English

Kuna matukio yanagusa sana mioyo yetu hivi kwamba hatuyasahau hata baada ya miaka mingi kupita. Kila mara unapokumbuka,  unapatwa na hisia za furaha zinazokufanya utabasamu. Labda unakumbuka zawadi uliyopewa ulipokuwa mtoto au uliposifiwa na mwalimu wako. Au furaha uliyopata mtoto wako mchanga alipotabasamu kwa mara ya kwanza

Je, ulijua kwamba kanuni hii inaweza kukusaidia kufanikiwa katika biashara yako? Wajasiriamali bora duniani wanatambua umuhimu wa kufurahisha wateja wao. Wanatafuta kila mbinu na ubunifu kufurahisha wateja wao kufikia kusema, “Kwa kweli nimefurahishwa na huduma bora unazotoa!”

Je, wewe hufanya hivyo katika biashara yako? Ikiwa hujaanza kufanya, soma na uchochewe na kampuni moja inayojitahidi kuhakikisha kwamba wateja wake wanahisi wanathaminiwa – kisha jifunze jinsi mbinu hiyo inavyofanya wapate wateja wengi zaidi. 

Hoteli Ndogo na ya Kawaida

Jiji la Hollywood lililo nchini Marekani linajulikana kuwa makazi ya waigizaji nyota wa sinema na eneo lenye bidhaa zinazouzwa kwa bei kubwa. Hivyo huenda ukashangaa kujua kwamba moja kati ya hoteli inayopendwa zaidi katika jiji hilo si hoteli ya bei kubwa na yenye anasa. Ni hoteli ndogo na ya kawaida inayoitwa Magic Castle Hotel.

Hoteli hiyo mwanzoni ilikuwa nyumba ya wakazi tangu mwaka wa 1950. Wamiliki wapya walibadili matumizi ya jengo hilo na kulipaka rangi ya njano inayong’aa, wakaweka viti kadhaa mbele ya dimbwi la maji na kuifanya iwe hoteli. Kusema kweli, ukilinganisha na hoteli nyingine katika jiji la Holywood hoteli hii haivutii. 

“Kwa nini hoteli hii inapendwa sana? Ni ya kizamani na si maridadi sana. Siri ni nini?”

Pamoja na hayo, hoteli hii ya kawaida katika jengo hilo la zamani imezungumziwa mara nyingi zaidi na wateja waliowahi kuishi hapo na kufurahia huduma. Maoni yao ni ya kuipendekeza hoteli hiyo na kuisifia kiasi cha kwamba kufikia sasa Magic Castle inashika nafasi ya 3 katika jiji hilo katika idadi ya watu wanaotoa maoni kuihusu kuliko hoteli nyingi za kisasa na zenye bei mbaya zaidi. Hii imewezekanaje? 

Simu ya Ice Lolly

Mkakati wa biashara uliofanya Magic Castle ifanikiwe ulitokana na wamiliki wake kujitahidi sana kuhakikisha kwamba wateja wao wanakuwa na “pindi zinazofurahisha.” Walitumia kila njia hata iwe ndogo kiasi gani kuwafurahisha wageni wao kwa kufanya mambo yaliyofanya watabasamu. 

Kwa mfano, wageni wanapofika, kitu cha kwanza wanachoona ni kaunta yenye vitafunio vitamu vinavyopatikana bure kwa wageni kwa muda wa saa 24. Ikiwa mgeni anasheherekea siku ya kuzaliwa, wanapewa zawadi na pongezi fupi ya maandishi wanapofika chumbani. Jambo la mwisho na muhimu, wana kitu maridadi kweli wanachokiita “Simu ya Popsicle.” 

Neno “popsicle” limezoeleka sana nchini Marekani nalo hurejelea aiskrimu au ice lolly. Ni barafu yenye utamu inayokumbusha watumiaji wengi nyakati za utoto wao. Magic Castle imebuni mbinu bora zaidi ya kuburudisha na kufurahisha wageni wao. 

Karibu na bwawa la kuogelea lililo hotelini kuna tangazo lenye Namba za Kupata Popsicle. Karibu na tangazo hilo kuna simu nyekundu ya kizamani iliyoning’inizwa ukutani. Kila siku kuanzia saa 2:30 mchana, mgeni anaweza kupiga simu hiyo na mfanyakazi wa hoteli atajibu na kusema “Habari, hapa ni kituo cha kutoa Popsicle, ungependa ladha gani?” 

Baada ya mgeni kutoa oda ya ladha anayopendelea, mfanyakazi aliyevalia glovu nyeupe na maridadi anatoka akiwa ameziweka katika sinia. Katika sinia hiyo kuna barafu ya lolly ya bure kabisa. Hata mgeni asiyependa kutabasamu hulazimika kutabasamu pindi tu anapoona mfanyakazi akitimua mbio huku amebeba sinia yenye barafu ya lolly inayotolewa bure. Ni jambo linalofurahisha, lisilotegemewa na linalopendeza sana.

Huduma Bora Haina Gharama Yoyote 

Jambo linalopendeza zaidi kuhusu yote hayo ni kwamba pindi kama hizo zinazofurahisha hazigharimu chochote. Wamiliki wa hoteli walitambua kwamba gharama ndogo watakayotumia kununua simu ya zamani na barafu za lolly ni ndogo sana ukilinganisha na faida watakayopata kutokana na kufurahisha wateja wao ambao watawaambia marafiki zao kuhusu hoteli hiyo. Hoteli hiyo si kubwa au yenye mbwembwe badala yake inavutia na inafanya wateja wasiisahau.  

Hakikisha Wanaiongelea Biashara Yako

Moja ya sababu inayoifanya Hoteli ya Magic Castle ifanya vizuri ni kwamba watu waliotembelea hoteli hiyo hawaachi kuiongelea kwa marafiki zao. Huduma waliyopata ni nzuri na ya pekee hivi kwamba wanamwambia kila mtu wanayemjua. Watu wanapoongelea biashara yako, hiyo ni mbinu bora zaidi ya kuitangaza bila malipo. 

Unachopaswa Kufanya Leo

Kama una biashara, fikiria mambo yatakayofurahisha wateja wako na kufanya wasisahau huduma zako. Kwa mfano, unaweza kubuni kitu kitachowafurahisha kama vile Simu ya Popsicle au  kitu cha ziada unachoweka kwenye kila oda wanayotoa au huduma bora ya wateja ambayo itawafanya waendelee kuizungumzia kwa marafiki wao wote.

 Kumbuka si lazima mambo hayo yakugharimu sana, jambo la msingi ni iwe kitu watakachokumbuka na kufurahisha wateja wako pamoja na kuwafanya wahisi wanathaminiwa katika njia ya pekee.

Ni mambo gani uliyojionea kwa wajasiriamali walio karibu nawe ambayo hutasahau? Mjasiriamali gani anakuvutia?

0
MAONI Sambaza

0 Maoni

Ili uandike maoni katika DreamLink ni lazima uwe umejisajili na umeingia katika akaunti. Tungependa kupata maoni yako hivyo acha tukusajili sasa!

Ingia