×
×

WANAWAKE JASIRI WANAOLETA MABADILIKO

Wanawake jasiri wanaoendesha MJ Piki hukabili vikwazo vyote njiani

Na Sakina Nanabhai

mj-piki-on-bikes-smiles
Swahili English

Karakana nyingi za kutengeneza pikipiki hujulikana kwa kuwa na harufu kali ya mafuta ya vifaa hivyo.

Utakuta hazina mpangilio, vitu chungu mzima vinavyohusiana na ufundi na visivyohusiana na ufundi vimerundikwa. Mwonekano huo unaendeleza dhana ya kwamba kazi hizo hufanywa na wanaume tu. 

Hali haiko hivyo ukitembelea karakana ya MJ Piki. Nilivutiwa sana na usafi na mpangilio wake. Pikipiki tano aina ya Honda zilizo safi na zenye rangi ya bluu iliyofifia zimepangwa katika mstari mmoja karibu na ukuta wenye nembo kubwa ya kampuni. Nilipofika nilipokelewa kwa uchangamfu na wanawake

Catherine, ambaye pikipiki yake inaendana na mwili wake mdogo, alinikaribia huku akinyoosha mkono wake na kusema “Hello, hello, hello!” Nilikaribishwa na  Rosemary, Jackline, na Spesioza waliokuwa wamekaa pembezoni mwa chumba. Nikavuta kiti na kujiunga na mazungumzo.Baada ya muda kidogo, Claire; kiongozi na mwanzilishi wa MJ Piki, aliingia na ndani na baada ya kukaa akaanza kunisumilia historia yake—jinsi MJ Piki, ambayo kirefu chake ni Mwanamke Jasiri ya Piki), ilivyoanza.

mj-piki-on-bikes

Jumuiya hiyo isiyo ya kiserilka inafanya kulingana na jina na lengo lake. MJ Piki inalenga kuwasaidia wanawake wanaotengwa na kunyimwa nafasi za kufanya kazi katika makampuni nchini Tanzania. Hawafundishi tu kila mtu bali wanakazia fikira katika kuwazoeza wanawake kuweza kuendesha bodaboda.  Kufanya hivyo huwawezesha wanawake kuwa jasiri na kufanya mabadiliko mpaka kutimiza ndoto zao.

“Nilitaka sana kufanya jambo tofauti. Ninashukuru sana nimekuwa sehemu ya MJ Piki na kuonyesha kwamba wanawake tunaweza,” akasema Catherine, akikumbuka alipoanza na MJ Piki. Katika harakati zake za kutumiza malengo hayo, alifanikiwa kuwavutia wengine pia. Rosemary anaongeza, “Wazazi wangu walikuwa wanaogopa kwamba nitapata ajali au jambo baya litanipata. Lakini tangu waliponiona nikiendesha pikipiki hawana wasiwasi na wananiunga mkono sana.”

Claire asingedhania kwamba jitihada zake za kutimiza ndoto zake miaka mitano iliyopita leo hii zingebadili maisha ya wanawake. Wazo hilo lilianza kitambo kidogo, pindi “nilipotumia karibu mwaka mzima nikiendesha pikipiki kutoka jiji la London mpaka Cape Town,” anakumbuka. “Pindi nyingine ilibidi kutumia njia zisizo rasmi ili kufika ninakoenda.” Alitumia kipindi hicho pia kufuatilia kwa ukaribu utunzaji wa pikipiki yake kwa kuwa “hilo ndilo jambo la pekee nililohitaji kufanya ili kuendelea kuwa salama katika safari yangu.”

Safari yake ilimfikisha Malawi ambapo aliamua kujitolea kufanya kazi na shirika lililofanya kazi ya kutunza na kuboresha pikipiki za wanachama wao. “Walikuwa na pikipiki 80 walizotumia katika kazi yao,” akasema. “Zilikuwa zikiharibika kila mara. Sababu kuu ya kuharibika ni kwa kukosa matunzo ya kutosha kwa hiyo nilianza kuwafundisha na kuwaonyesha jinsi ya kutunza na kudumisha magari na pikipiki ili kuwa salama barabarani.” Mwongozo wa Claire uliwanufaisha sana ndio maana alichochewa kutoa mafunzo kama hayo mara baada ya kuanza kuishi Tanzania.

Claire-with-mj-piki

Malengo ya mafunzo yake yalikua zaidi baada ya kuombwa kutengeneza pikipiki 2 kati ya 400 zilizokuwa zikitumiwa kama magari ya wagonjwa Sengerema. Pindi hiyo, Claire aligundua kwamba kuna nafasi kubwa ya kuwafundisha wanawake kuendesha pikipiki ili kutoa huduma huduma hiyo, “kuanzia hapo wanawake hawa unaowaona walijiunga,” akasema akirejelea wanawake waliokuwa pembeni yake.

“Wanawake wa hapa ni wachapa kazi na wanafanya mengi ili kuruzuku familia zao. Kuna wanawake wanaofanya kazi ya kuuza chakula au kushona nguo na wakati huo huo wanalea watoto wao na mambo mengine.” Anatabasamu na kujivunia wanawake hao wenye bidii. “Nimekutana na wanawake walioniambia, ‘Nikipata nafasi ya kuendesha pikipiki, ningependa kufanya hivyo na kuleta mabadiliko.’ Nikafikiri, lingekuwa jambo linalofaa kuwapa nafasi hizo wanawake na kisha kuona kama kuna mwanamke atakayejiunga.”

Wazo hilo likafungua nafasi nyingi za kujiendeleza kwa wanawake na MJ Piki. Leo hii shirika hilo lina lengo la kuunga mkono vikundi kadhaa vyenye nia ya kuanzisha huduma ya kupeleka wagonjwa kwa kutumia pikipiki, “hususa kusaidia wanawake wajawazito na wanaokaribia kujifungua,” Claire akaongezea. “Kuna idadi kubwa ya vifo vya mama wajawazito Tanzania na sababu kubwa ni wanawake wengi hawafikishwi hospitalini kwa wakati.”

MJ Piki ina mipango ya kuanzisha pikipiki zao wenyewe zitakazotumika kama magari ya wagonjwa ili kutatua tatizo hilo Tanzania. Kwa kuwasaidia wanawake hao kujiajiri kupitia kutoa huduma hiyo ya kuendesha bodaboda, Claire anaamini kwamba akina mama katika mkoa huo watakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kujifungua salama bila matatizo yoyote yanayotokana na ukosefu wa usafiri.

Ni faida pia kwa Claire mwenye mtoto mdogo wa kiume. Alipoanza kulia tulipokuwa tukimalizia mazungumzo yetu, aliamua kuvuta kigari alichombebea karibu naye. Huku akicheka na kuvuta kigari karibu na kifua chake, Claire akasema, “Ningependa kukutambulisha kwa mwanachama mdogo zaidi wa MJ Piki, Bwana Benjamin.”

mj-piki-bike-mirror

Ingawa kulea humfanya awe na mambo mengi, Claire hana mpango wa kupunguza jitihada zake za kuijenga MJ Piki. Catherine, Rosemary, na Jackline pia wanafanya kila jitihada ili kuboresha shirika lao wakiwa na  lengo la kuchochea wanawake wenzao.

“Mara nyingine ni changamoto unaposikia watu wakisema maneno kisa tu wewe ni mwanamke. Watu wengi huniambia ‘Utagonga,’” Catherine akasema.

Na ni kweli, karibu wote wamewahi kuangua mara nyingi tu. “Lakini kwa kuwa naipenda kazi yangu na nina hamu ya kuwa bora zaidi sikuacha kufanya mazoezi mpaka nilipoweza kuendesha vizuri,” akaongeza Rosemary.

Walijaribu na kuanguka na kuumiza miguu yao. Hata hivyo, watu wanapowaambia kuacha wao husimama, hufuta mavumbi kutoka katika nguo zao na kufuta mafuta kutoka mikono mwao. Na tofauti na matarajio ya wengi, wanaendelea kufanya mengi bila kikomo.

Maelezo Kuhusu Mwandishi

sakinakavi@yahoo.com

Sakina Nanabhai:

Hey there! This is Sakina. I am a full-time mommy and a freelance journalist. I spend most of my days pampering and absolutely spoiling my little toddler girl, Lubaina. (Remember the name because I talk a lot about her). Once she is off to bed, I spend my nights hammering down my laptop keys, and writing articles. I love interviewing and meeting new people. Having interviewed Tanzanian multi-millionaires, fashion designers, models, artists and a lot of famous personalities in the past, with Dreamlink I wish to reach out to the 'ordinary' women of Tanzania with extraordinary stories of courage and perseverance. Dreamlink came across as a dream-come-true opportunity to work with like-minded people with crazy ideas and ambitions, and who dare to make their dreams come true, by daring to dream! Happy to connect with you to know about your dreams that don’t let you sleep at night.

0
MAONI Sambaza

0 Maoni

Ili uandike maoni katika DreamLink ni lazima uwe umejisajili na umeingia katika akaunti. Tungependa kupata maoni yako hivyo acha tukusajili sasa!

Ingia