×
×

MBINU BORA YA BIASHARA YA MFANYAKAZI WA BENKI MTENGENEZA GELATO

Mercy Kitomari, ambaye biashara yake ilishinda tuzo kubwa na mafanikio yake kutangazwa na vyombo vya habari vya kimataifa kama BBC anatoa ushauri kwa wajasiriamali watarajiwa

Na Ayushi Ramaiya

Swahili English

Ni tamu na yenye kuvutia iliyowekwa viungo vya nyumbani. Ina ladha ileile na ubora wa hali ya juu…  

Tuliwaza hivyo tulipokuwa tukijaribu gelato ya Mercy Kitomari. Tulikuwa  na maswali mengi kuhusu ladha, mchanganyiko na kilichomchochea kuanza biashara hiyo. Hata hivyo, pindi yote hiyo swali moja lilikuwa la muhimu zaidi kwetu.

“Utapata wapi hapa Tanzania gelato (ice cream) hii?”, tulimuuliza.

Mercy, mwanzilishi wa Nelwa Gelato, kampuni iliyoshinda tuzo alikuwa tayari kutujibu kwa shangwe.

“Utapata katika hoteli kadhaa zenye hadhi ya nyota tano jijini Dar es Salaam na katika maduka yanayouza ice-cream nchini Tanzania,” akatujibu. 

Mercy anaishi katika nyumba ya kawaida bila ghorofa eneo la Magomeni, ambapo anafanya biashara yake ya kutengeneza gelato yenye matunda na kuwafundisha wajasiriamali wapya. Sebule yake imejaa vitabu upande mmoja na majokofu yenye ice cream upande mwingine. 

Anapokuwa hatengenezi ice cream, hutumia wakati wake kuboresha biashara yake kwa kufanya utafiti kwenye mtandao kwa kutumia kompyuta yake jikoni. Ofisi yake ni korido iliyojaa mashine anazotumia kutengeneza gelato zenye kiwango kikubwa cha ubora zinazopendwa na watu wengi Tanzania.

Kila mtu anatengeneza ice cream.  Zako zina tofauti gani? 

Mercy:  Watu waliofanikiwa katika biashara hufikiri kwa sauti. Nilikuwanikiandika ripoti yangu ya shahada ya pili au MBA huko nchini Uingereza kuhusu je ni kitu gani kinachomwezesha mtu kununua ice cream. Nilipokuwa nikiandika ripoti hiyo niligundua kwamba kuna jambo limekosekana nchini kwetu. Nchi hii ni ya kitropiki yaani ina joto, hivyo ice cream inapaswa kuwa bidhaa kubwa kutumiwa. 

Ni gharama sana kuendesha biashara hii lakini nilitafuta njia badala kufanikiwa. Nilianza kwa kutumia mashine zilizotengenezwa mchini China. Nikafuata mbinu nilizofundishwa na mpishi mmoja nchini Uingereza na nikajiunga na Chama cha Wapishi Tanzania. 

Mimi si wa kwanza au wa pekee lakini jambo linalonifanya niwe tofauti ni kwamba ninafikiria tofauti. Nimenunua matunda, karanga na viungo kutoka sokoni na kutumia mchanganyiko huo kutengeneza gelato bora zaidi nchini Tanzania. 

“Mimi hufikiria kwa marefu na mapana au picha nzima na hilo hunisaidia sana.Huamua mambo yote na mara nyingi ‘hapana’ yangu mara nyingi huwa ‘ndiyo’ yangu baadaye.Mimi hushughulikia hali yoyote iliyo kama kikwazo ili kutimiza malengo yangu.”

Kutojiamini ni tatizo la kawaida kwa wajasiriliamali wengi. Una ushauri gani?

Mercy: Siku moja rafiki yangu aliniambia, “Kuna mawazo mengi ya biashara katika dunia hii na kwa kawaida hukuchagua ili kuona ni kwa kiasi gani unataka kuyatumia na kupata mafanikio. Ukiyakubali na kuyafanyia kazi yatakuwa pamoja nawe. Ukijishuku kila mara, yataondoka na kumtafuta mtu mwingine.” Kila siku ninafanya maamuzi yanayohusisha kujishuku au kutojiamini kama vile ninapochagua shati ya kuvaa au ninunue au nisinunue gari mpya. Hata hivyo mimi hujiuliza, ‘Kuna sababu yoyote ya kuruhusu kujishuku huku kuniamulie maisha yangu?’ 

“Kila siku ni lazima uchague kupigana ili kutimiza malengo na ndoto zako, usikazie fikira changamoto ndogo ndogo na jiwekee lengo la kutimiza mambo makubwa. Ni pambano la kila siku.” 

Mbali na majaribio na kushindwa, je, kushindwa kunakuogopesha? 

Mercy:  Kutengeneza ice cream ni jambo linaloleta furaha kwa hiyo sina haja ya kuwa na sura ya kazi!

Baadhi ya changamoto nilizopata mwanzoni katika biashara hii ni kuvunjika moyo na kuugua kila mara. Ninamejinyima mambo mengi sana kufikia sasa ili kutimiza ndoto zangu. Baada muda nimeweza kutohusisha maisha yangu binafsi na biashara yangu.

Nimetumia nafasi hiyo kama njia ya kujifunza bila kuhusisha hisia. Ninaposhuka moyo mimi hukaa chini na kuandika jinsi ya kuboresha biashara yangu na kufanya yote niwezayo kufanikisha mpango huo. 

“Usipumzike mpaka utakapopata mafanikio. Kushuka na kupanda kutakufanya uwe bora hata zaidi katika biashara yako. Jambo la muhimu ni kutimiza lengo lako hivyo usikate tama hata kidogo bali endelea kupambana.”   

Pindi ambazo hupati faida, je, wewe hupunguza ubora wa bidhaa zako? 

Mercy: Ubora wa bidhaa ndilo jambo la muhimu zaidi bila kujali ni biashara gani unafanya. Kama haudumishi ubora hautafanikiwa. Naweza kutengeneza ice cream kwa kuweka sukari na maziwa kidogo au kutumia ladha ya matunda aina ya strawberry badala ya matunda yenyewe, lakini mimi hujiuliza “Nitafanikiwa kweli nikianza kudanganya?”  

“Ubora una gharama zake, lakini utakulipa baadaye. Kupunguza ubora wa biashara yako utagharimu mafanikio yako.” 

Je, mtu atapataje faida?

Mercy: Kama wewe ni mtu wa kutaka mafanikio ya haraka hautafika mbali. Kumbuka kwamba mbegu bora unayopanda sasa ndiyo itakayozaa. Kuwa chanzo cha mabadiliko na kugusa maisha ya watu kwa kuleta jambo tofauti. 

Mafanikio yetu hayapimwi na kiasi cha fedha tulichopata bali namna tulivyoleta mabadiliko katika maisha ya watu. Fedha hukufuata. Jiulize, umeacha nini ili kufanikiwa? Unaweza kupata pesa kwa urahisi tu lakini unapofanya kazi kwa bidii na kujidhabihu, utaanza kuona thamani ya pesa uliyopata.  

“Kila siku ninaboresha safari yangu ya kupata mafanikio. Nilipoanza kuwekeza zaidi katika biashara hii, nilipokosea, nilipofanya jambo jipya, nilipopata zaidi faida kuliko jana ndipo nilipogundua kwamba ninakua kibiashara.”

 

Unakabilianaje na changamoto? 

Mercy: Mimi hutoa maoni yangu na mawazo kuhusu biashara yangu. Kufanya hivyo kumenisaidia kukua kutoka kuuza ice cream mpaka kuanza kufundisha watu nchini Tanzania jinsi ya kutengeneza gelato ya Nelwa ambayo imepata mafanikio makubwa kufikia sasa. Usikalie ujuzi wako badala yake waambie wengine mawazo yako ya biashara. Kuwa mwerevu na panua biashara yako. Ikitokea unasifiwa kwa mafanikio yako, usibweteke na kuhisi kwamba umefika bali boresha zaidi. 

“Ongea na watu. Watu ni kama dawa. Utafaidika sana kwa kuongea na watu na utakumbushwa kuhusu utu wako, Utasaidiwa pia kutoacha kutimiza ndoto zako.”

Kutimiza lengo lako ndiyo mwisho wa kutimiza ndoto zako? Umefikia wapi katika hilo? 

Mercy: Mwisho wa siku lengo langu kuu ni kuona Gelato ya Nelwa inatambuliwa kama mzalishaji mkuu nchini Tanzanian wa gelato ice cream inayopendwa zaidi. Ninataka mtu akifika Tanzania, jambo la kwanza na muhimu kwake liwe kujaribu Nelwa Gelato. Nataka wateja wangu wawe wakisema, “Kama haujatumia gelato ya Nelwa basi bado haujatumia ice cream.” Hii ni ndoto yangu kubwa na kwa sasa ninashirikia na watu ili jina langu litambuliwe zaidi kupitia watengeneza ice cream ninaoshirikiana nao. Sijaridhishwa na idadi hivyo ninaendelea kupambana ili kuongeza idadi. 

“Kila mtu hufafanua mafanikio kwa njia yake. Lengo langu ni kujenga jina la kampuni yangu ambalo halisahaulika hata baada ya miaka mia moja wala si baada ya kununua gari kubwa. Mtazamo wangu kuhusu mafanikio umebadilika kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mwanzoni.” 

Ungependa kuwaambia nini wanawake wanaotaka sana kuanzisha biashara? 

Mercy:  Mafanikio hufafanuliwa na mambo mengi na sababu inayokufanya ufanye kazi hiyo. Kama unafanya biashara ili kujionyesha basi ni bora usiendelee. Hata hivyo kama unafanya kwa sababu unataka sana kufanya biashara hiyo basi ifanye. Kama wewe ni mwanamke unayeamini kwamba unaweza kufanya mambo mengi kutimiza ndoto zako na haujali maoni ya jamii inayokuzunguka basi usiache kufanya biashara hiyo kuanzia leo. 

Ni kweli itabidi ujidhabihu sana katika maisha yako binafsi, hata hivyo kumbuka kwamba hakuna linalowezekana bila kujidhabihu. Uwe tayari kukabiliana na hali hiyo ili kutimiza lengo lako. 

“Hakuna jambo linaloumiza kama kuishi maisha ya mtu mwingine.”

Maelezo Kuhusu Mwandishi

Ayushi Ramaiya

Ayushi Ramaiya:

Hi! I am Ayushi, a journalist based in Dar es Salaam. I am an advocate of social change and positive media. My dream is to own a travel channel.

0
MAONI Sambaza

0 Maoni

Ili uandike maoni katika DreamLink ni lazima uwe umejisajili na umeingia katika akaunti. Tungependa kupata maoni yako hivyo acha tukusajili sasa!

Ingia