×
×

KUTENGENEZA MAISHA BORA KUPITA KILA MSHONO

Mradi wa Lulu huwawezesha wanawake kupitia sanaa na elimu

Na Sakina Nanabhai

Swahili English

Ni rahisi kufikiri makao makuu ya Mradi wa Lulu (TLP) ni kanisa unapoingia ndani yake kutokana na msalaba mweupe uliotundikwa katika kuta zake.

Hata hivyo unapopanda ngazi kuelekea juu unaanza kuona unamna-namna tofauti unaokusaidia kupata picha kamili ya kinachoendelea katika makao makuu hayo. 

Katika chumba hicho utakuta nguo nyingi za watoto zilizotengenezwa kwa kitenge, blanketi na urembo pamoja na midoli iliyotengenezwa na wasichana katika vikundi kati ya 10-20 wanaofanya kazi pamoja ili kuboresha stadi zao na kufaidisha jamii yao. 

Corine ’t Hart, ni mwanzilishi na kiongozi wa TLP, taasisi inayofanya kazi ya kubadili nguo kuwa sanaa yenye kuvutia vinavyouzwa hatimaye. “Hizi ni baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa sana na akina wanawake tunaofanya nao kazi,” anasema akirejelea mdoli aina ya teddy bears, viboko na twiga waliotengenezwa kutokana na vitenge. 

Tofauti na mtu anavyoweza kufikiri, Corine—aliyehamia Tanzania miaka nane iliyopita—alisema kwamba hakujua jinsi ya kutengeneza bidhaa hizo alipoanzisha TLP. Tangu utotoni alitaka sana kusaidia binadamu wenzake baada ya familia yake kuwa na kawaida ya kutunza watoto waliopewa na Shirika la Msalaba Mwekundu nyumbani kwao nchini Uholanzi wakati wa likizo ya majira ya kiangazi na kupitia elimu aliyopata ya Masomo ya Bara la Afrika. Alipounganisha mambo hayo mawili kuhusu maisha yake alipokuwa akianzisha TLP, aligundua mara moja kwamba kuna jambo la muhimu lililokosekana ambalo wakati huo hakulifahamu vizuri.

“Ili niweze kuwafundisha wasichana ilikuwa lazima nijifunze mambo hayo kwanza,” akatabasamu. “Tulianza kwa kutazama video za YouTube kisha tukawafundisha wasichana.” Leo, wakufunzi 26 wa TLP “hutunza vikundi hivi na kuhakikisha kwamba wasichana hao wanajifunza stadi vizuri ipasavyo.”

Ufundi ni mwanzo tu. Mbali na hilo, wasichana wa Lulu hufundishwa jinsi ya kuwa na maisha bora, kutunza na kutumia pesa, afya na ujasiriamali. Ikiwa sehemu ya shirika la Society of African Missions (SMA), asasi ya kanisa la Katoliki inayoshughulikia kuboresha hali za wasiojiweza, Corine aliombwa kufanya kazi na wasichana walio na umri kati ya miaka 15-25. Mradi wa Lulu hutumia ubunifu wake kwa lengo kubwa zaidi: kuwawezesha wale wanaowafikia ambao kwa namna moja au nyingine hawajiwezi.

Nchini Tanzania, kundi la wasichana wenye umri huo liko hatarini kufuata maoni ya jamii inayowazunguka. Wasichana wengi wanapofika umri huo huacha shule kwa sababu ya kupata mimba. Wengine hulazimika kubaki nyumbani ili kutunza nyumba kwa sababu familia imesema. 

Kupitia jitihada za vikundi kama Mradi wa Lulu, Corine analengo la kubadili mtazamo huo kiasi cha kuwazuia wanawake wengine nchini Tanzania kwa muda mrefu. Tangu kuanzishwa kwa Mradi wa Lulu miaka sita iliyopita alipohamia nchini, Corine amepata mafanikio na anatarajia mambo mengi mazuri wakati ujao. 

“Kumekuwa na itikio zuri,” ankasema. “Familia nyingi hufurahia sana kuona kwamba hata ingawa wasichana wao walishindwa kuendelea na shule au walipata ujauzito bado wamepewa nafasi ya pili katika kuberasha maisha yao.” Pamoja na hayo wakati mwingine anasema, wasichana huonekana kuwa mali na kuna baadhi ya familia zinazopinga jitihada zozote tunazotoa za kumsaida msichana huyo kwa kuwa anapaswa kufanya ‘kazi za nyumbani.’ “Wanatarajiwa kufanya kazi karibu zote za nyumbani kama vile kulea wadogo zao,” Corine akasema. “Au hawawezi kuondoka nyumbani na kuwaacha watoto na waume zao.”

Kwa sababu hizo, kazi ya Corine haihusishi tu kuwafundisha wasichana wa Lulu kufuma blanketi na vifungo bali pia kuzungumza na wazazi na kujaribu kuwashawishi kuruhusu wasichana wao kutimiza ndoto zao na kujifunza stadi zitakazowasaidia maishani huku wakitumia wakati unaobaki pamoja na familia zao.

“Ni jambo la muhimu kuwawezesha wasichana mapema iwezekanavyo ili wanapokuja kuwa na familia zao hawatahitaji kutegemea mtu ili kupata riziki ya kila siku na wawe na uwezo wa kujitegemea wenyewe kihalali,” akaongeza Corine. 

Msichana anajua kwamba muda na matunzo huhitajika katika kushona kitu mpaka kifikie hadhi ya kuuzwa. Corine huchochewa pia na wasichana waliofanya vema maishani kwa sababu ya ujuzi walioupata kupitia kushirikiana na TLP. Alituonyesha msichana anayeitwa Elizabeth, ambaye kwa mbali anaonekana akifanya kazi katika kompyuta ndani ya ofisi. Alikutana naye “alipokuwa amemaliza kidato cha nne,” Corine anakumbuka huku dhahiri akionekana kujivunia maendeleo ya Elizabeth.. “Alitaka kujifunza mengi zaidi na muda si muda akawa mtu wa muhimu sana katika mradi wetu.” 

Kufikia sasa, Elizabeth ni mshiriki wa zamani zaidi wa TLP na hushughulikia masuala ya utawala mbali na kazi yake akiwa mwezeshaji. Kwa sababu ya kazi nzuri inayofanywa na TLP, simulizi lake ni mojawapo kati ya masimulizi mengi yanayounganisha wasichanana nchini Tanzania katika kutimiza malengo yao ya wakati ujao. 

Kwa habari zaidi kuhusu Mradi wa Lulu temblea ukurasa wao wa Facebook wa www.facebook.com/luluproject

Maelezo Kuhusu Mwandishi

sakinakavi@yahoo.com

Sakina Nanabhai:

Hey there! This is Sakina. I am a full-time mommy and a freelance journalist. I spend most of my days pampering and absolutely spoiling my little toddler girl, Lubaina. (Remember the name because I talk a lot about her). Once she is off to bed, I spend my nights hammering down my laptop keys, and writing articles. I love interviewing and meeting new people. Having interviewed Tanzanian multi-millionaires, fashion designers, models, artists and a lot of famous personalities in the past, with Dreamlink I wish to reach out to the 'ordinary' women of Tanzania with extraordinary stories of courage and perseverance. Dreamlink came across as a dream-come-true opportunity to work with like-minded people with crazy ideas and ambitions, and who dare to make their dreams come true, by daring to dream! Happy to connect with you to know about your dreams that don’t let you sleep at night.

0
MAONI Sambaza

0 Maoni

Ili uandike maoni katika DreamLink ni lazima uwe umejisajili na umeingia katika akaunti. Tungependa kupata maoni yako hivyo acha tukusajili sasa!

Ingia